MABONDIA KUPIMA UZITO IJUMAA STEND YA BAGAMOYO KWA AJILI YA MPAMBANO WA JUMAMOSI

NGUMI KUPIGWA MEI 16 BAGAMOYO MJINI

 

 

Na Mwandishi Wetu 

MABONDIA Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo na Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam watapima uzito siku ya ijumaa katika stendi kuu ya mabasi Bagamoyo na kupigana siku ya jumamosi ya mei 16 katika ukumbi wa che kwa che 

uliopo Bagamoyo mjini ambapo mabondia hawo watamalizia ubishi wao wa nani zaidi kati ya bagamoyo na Chanika

mpambano uho utakaosimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa P.S.T litakuwa la raundi sita na kg 61 ambapo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi siku hiyo yatakayowakutanisha bondia

Rashidi Haruna atakumbana na Kaminja Ramadhani na Harid Hongo atakabiliana na Kishoki Mbishi mpambano mwingine ni Abdallah Samata atakaye zidunda na Maono Alli 

mipambano hiyo inaletwa kwenu na Sharif Promotion wakati mgeni rasmi siku hiyo ni bondia kutoka morogoro Cosmas Cheka ambaye atakuja kuwapa nasaa mbalimbali mabondia na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuweza kusonga mbele kwa mchezo uho mjini Bagamoyo

kingilia katika mpambano uho ni Tsh, 8000 kwa V.I.P na kwaida ni sh. 5000

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na upatikanaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar vs Manny Paquaio 2015 , Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikigawiwa na kocha  Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha mchezo wa masumbwi nchini
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List