Rais Pierre Nkurunziza yuko wapi?

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akiwa na Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi kabla ya jaribio la mapinduzi
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, inasemekana ameondoka nchini Tanzania saa moja baada ya kupatikana taarifa za kupinduliwa kwake na kiongozi mkuu wa majeshi yake Meja jenerali Godefroid Niyombare kutangaza kwamba amempindua.
Jenerali huyo mara baada ya tangazo lake, akaweka amri ya kufungwa kwa kiwanja cha kimataifa cha ndege nchini humo ikiwemo mipaka ya Burundi.
Hata hivyo haiko wazi ikiwa jeshi linamuunga mkono generali Meja jenerali Godefroid Niyombare.naye msemaji wa rais wa Burundi ,amesema kwamba wanajeshi watiifu kwa Rais ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa viongozi nchini Tanzania,amesema nchi iko shwari.
Maelfu ya watu wamekuwa katika shamra shamra katika mji mkuu wan chi hiyo Bujumbura baada ya wiki kadhaa za maandamano kumpinga katika maamuzi yake ya kugombea muhula wa tatu wa uongozi,na tayari mpaka sasa viongozi wakuu wa kanda wamelaani mapinduzi hayo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List