SERIKALI YAOMBWA KUBORESHA MIUNDOMBINU.Wakazi wa mtaa Gome kata mzingani wilaya ya Tanga wameiyomba serikali kutengeneza miundombinu ya mfereji maarufu kwa jina la Mfereji Mama unaotumika kusafirisha maji machafu kutoka katika viwanda yenye kemikali,Maji hayo siku za nyuma yalisababisha maafa kwa wakazi kwa kupoteza viungo na matatizo ya ngozi.

Kutokana na mvua zinazo endelea maji hayo yametoka katika mkondo na kusambaa katika makazi ya watu na kusababisha baadhi kukimbia makazi yao.Ambapo hata shughuli za kila siku zimekuwa ngumu kutokana na uwepo wa maji hayo kama wanafunzi kushindwa kwenda shule.

Pia wamewatupia lawama viongozi wa eneo hilo kwa kufimbia macho eneo hilo na kuomba Viongozi wa ADC kuboresha eneo hilo kwa kuwapa nafasi katika uchaguzi unaokuja.KATIBU wa wanawake ADC Tanga na Mjumbe wa bodi ya uongozi Taifa Bi:Asha Juma amejitokeza kutangaza nia ya kugombea Udiwani ili aweze kutatua kero hiyo inayowakabili wakazi wa eneo hilo.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List