BONDIA ABDALLAH PAZI NA IMAN MAPAMBANO KUPANDA ULIGONI IDD PILI Promota wa Ngumi za Kulipwa, Shomari Kimbau (katikati) akiwa ameshika mkanda ambao utapiganiwa na bondia Abdallah Pazi (kushoto) na Iman Mapambano (kulia) kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni siku ya Idd pili katika uzito wa kilo 76 light heavy raundi 10. (Picha na Rahel Pallangyo)

BONDIA Abdallah Pazi anatarajiwa kupanda ulingoni Idd Pili kwenye ukumbi wa Vijana Kinondoni kuchuana na Iman Mapambao katika pambano la ubingwa wa Taifa lililoandaliwa na promota mkongwe Shomari Kimbau chini ya Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kimbau alisema Pazi atapambana na Mapambao katika uzito wa kilo 76 light heavy raundi 10 ambapo mshindi atapambana na Mkenya Daniel Wanyonyi katika pambano la Afrika Mashariki litakalofanyika mwezi ujao.
 “Maandalizi yanakwenda vizuri, tunategemea pambano litakuwa la kuvutia kutokana na kuwaleta mabondia vijana wenye uwezo ambao watakuwa tegemeo baadaye katika mapambano ya kimataifa,”alisema.
Alisema katika kuboresha na kuhamasisha michezo mshindi wa pambano hilo la ubingwa atavalishwa mkanda wa taifa na Diwani wa Kata ya Mwananyamala Songoro Mnyonge.
Aidha, aliwataja mabondia wasindikizaji kuwa ni Rahim Maokola atachuana dhidi ya George Demoso uzito wa kilo 60  L/middle, Shabani Kaoneka dhidi ya Sweet Kalulu  uzito wa kilo 72 middle weight  raundi nane na  Chid Mbishi dhidi ya Mbwana Mdani  uzito wa kilo 52 Flyweight raundi sita.
Wengine ni Aman Mssy dhidi ya Peter Nunda uzito wa kilo 86 heavyweight raundi nne na Hans Mawe dhidi ya Bakari Chuma wenye uzito sawa na huo.
Kimbau alisema amerudi kwenye ngumi baada ya kuona kuwa TPBC imesajiliwa chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili kuwasaidia mabondia chipukizi kutimiza ndoto zao.
“Nawashukuru sana BMT kwa kuisajili TPBC kwani kufanya hivyo ni kutambua na kuunga mkono kazi ambazo tumekuwa tukizifanya katika kuendelea mchezo wa ngumi nchini, tunakuja kwa kasi kuandaa mapambano mbalimbali ili kuibua wengine wasiofahamika,”alisema.
Alisema yeye ndiye aliwaibua mabondia wakubwa kama Kalama Nyilawila na Mada Maugo hivyo kitendo cha kurudisha kasi kwa mabondia hao chipukizi kutawaimarisha viwango vyao.
Alisema baada ya pambano hilo, anatarajia kuandaa  mengine nane na kushirikisha mabondia tofauti kwa lengo la kupata mabondia 10 bora.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List