ADC LUTAYOSA YEMBA NDIE MGOMBEA WA URAIS WETU.

Chama cha Alliance for Democratic Change ADC kimempitisha Lutayosa Yemba kuwa mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Huku Mwenyekiti wa chama hicho Said Miraji Abdallah akiteuliwa kuwa mgombea mwenza,ambapo kwa upande wa Zanzibar utawakilishwa na Hamad Rashid Mohamed aliyekuwa Mbunge wa Wawi.

Hatua hiyo imefuatia baada ya Wajumbe wa chama hicho kuwathibitisha wagombea hao kwenye Mkutano Mkuu wa Chama,ambapo vipaumbele kwenye Irani ya chama vikiwa ni kusimamia haki,Usawa,Utu na kuilinda amani ya nchi.

Akifungua mkutano Mwenyekiti wa ADC Taifa Said Miraj Abdalah amesema ili maadhimio hayo yatimie watahakikisha wanatoa Elimu kwa mpiga kura ili aweze kuchagua mtu sahihi atakayeleta maendeleo ya nchi na siyo kuangalia chama.

Kwa upande wake Mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Chief Lutayosa Yembe amesema sekta ya afya na maji ndiyo vipaumbele vyake vya kwanza endapo atapata nafasi hiyo kutokana na umuhimu wa huduma hizo.Naye Mgombea urais kwa Zanzibar kupitia chama hicho amezungumzia suala la uchumi kwa namna ya kipekee katika kuleta mabadiriko.

Hatua ya chama hicho cha ADC kuwapitisha wagombea urais kwa Tanzania bara na Zanzibar ni miongoni mwa michakato inayoendelea kwa baadhi ya vyama vingine vya siasa wakati ikiwa inaelekea katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika October 25 mwaka huu.

















Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List