CHADEMA IMEKUBALI LOWASSA KUWA MGOMBEA URAIS KWA CHAMA HICHO.

Baraza kuu la CHADEMA limeridhia waziri Mkuu aliyejiuzulu Ndugu Edwad Lowassa kugombea urais kupitia chama hicho,na Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA huku aliyekuwa waziri wa afya Zanzibar kpitia chama cha wananchi CUF Ndugu Juma Hajji Duni akipitishwa kuwa mgombea mwenza.

Hatua inafuatia makubaliano ya mkutano mkuu wa CHADEMA baada ya kujiridhisha kwamba Edward Lowassa ndiye chaguo la Watanzania atakayetimiza ndoto ya upinzani kushika dola.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema ni lazima kujitoa muhanga ili kutimiza ndoto ya upinzani kuleta mabadiliko bila kujali maslahi binafsi.Pia amegusia suala la ukimya wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa kuwa ni makubaliano apumzike kwa mda lakini nafasi yake ipo palepale.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa wenyeviti wa Mikoa CCM,mgana Msindai aliyejiunga na CHADEMA ameelezea sababu za kujiengua na CCM huku Mwenyekiti mwenza wa UKAWA na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia akielezea uteuzi wa Lowassa ndo suluhu ya UKAWA kushika Dola.











Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List