Dr John Pombe Magufuli Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Wa Kiti cha Urais wa Tanzania

 Dr John Pombe Magufuli Atangazwa Rasmi Kuwa Mshindi Wa Kiti cha Urais wa Tanzania kwa Asilimia 58.46
Tume ya uchaguzi ya Tanzania Bara (NEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji Damian Lubuva imemtangaza Rasmi mgombea Urais wa CCM, Dr John Pombe Magufuli kuwa mshindi halali wa kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili wiki iliyopita.
Kwa Mujibu wa jaji Lubuva, Dr magufuli amepata ushindi wa kura Milioni 8 ( 8,882,935 ) sawa na asilimia 58.46% huku akimwacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu , Edward Lowassa (Chadema ) ambaye amepata jumla ya kura Milioni 6 ( 6,077,848 ) sawa na asilimia 39.97%
Dr Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu watakabidhiwa rasmi vyetu vya ushindi kesho saa nne asubuhi katika ukumbi wa hoteli ya Diamond Jubilee
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List