Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa wametoa wito kwa baadhi ya Watanzania kuacha kuwanyoshea Vidole baadhi ya Mawaziri na Manaibu waliochaguliwa jana na Rais Dk John Pombe Magufuli badala yake wawape muda ili wawapime kwa utendaji kazi wao. Wito huo umekuja baada ya Rais Magufuli kuteua Baraza la Mawaziri na manaibu waziri 34. Katika uteuzi kumekuwepo na maoni tofauti huku wengine wakihoji uadilifu na dhamira ya dhati ya wateule hao lwapo wataweza kuwa wazalendo kama Rais Magufuli. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Abdullah Bulembo akiwataka Watanzania kushirikiana na viongozi wa Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha dhamira ya Rais Magufuli inatekelezeka
DKT. YONAZI TUKO TAYARI KWA CHAN 2025
-
Dkt. Jim Yonazi aongoza makatibu kukagua viwanja,asema sasa Tanzania
timamu kwa CHAN .
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt....
Saa 11 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni