WANANCHI WAISHIYO KIJJI CHA MWANDEGE KATA MWANDEGE WILAYA YA MKURANGA PWANI WAMEMUOMBA MWEKEZAJI WA KIWANDA CHA AZAM ASIKIE KILIO CHAO NYUMBA ZAO ZINABOMOKA NA MAJI YA MVUA YANAYOPITA KUTOKA KWENYEMFELEJI WA KIWANDA HICHO CHA AZAM

Wananchi hao wamesema wamekuwa wakiishi kwenye maeneo hayo zaidi ya miaka 40  kulikiwa na mfereji mdogo ambao Maji yake yalikuwa ni madogo pia hayana nguvu Kutokana na mfereji huo kuwa na Maji kidogo hata kipindi cha Mvua. Lakini katika miaka ya hivi karibuni baada ya kujengwa kwa Kiwanda cha Azam kumekuwa na Kelo ya miundombinu kuaribika wakati Mvua inaponyesha. Wananchi hao baada ya kuona Mfereji huo ukizidi kupanuka na kuwa Mto na kuleta athari za Nyumba kubomoka waliamua kufatilia cha Mfereji kugeuks Mto ndipo walipogundua Maji hayo kipindi cha Mvua yamekuwa mengi Kutokana na Mtaro wa. Maji ya Kiwanda kuelekeza katika makazi ya Wananchi. Bi Hadija Mkumba ni Mjane ambaye aliachiwa Nyumba na Marehemu Mume wake imebomoka na Kubakia na chumba kimoja cha Kulala yupo katika wakati mgumu wa maisha jinsi ya kuishi na Watoto wakiume na wakike wakubwa katika chumba kimoja. Bwana Rajabu Mpanzi na BI Pili Mkaza wote nao nyumba zao zimebomoka huku wakiofia mvua zinazoendelea kunyesha wanaweza kuatalisha maisha yao na Watoto. Mjumbe shina namba 25 Mwandege Ally Abdallah amesibitisha kutokea kwa Maji mengi kipindi cha Mvua yanayotaka katika Kiwanda cha Azam. Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Mwandege Ally Hasumani Ubuguyu na Mwenyekiti wa Kitongoji Mwandege Mjini Hassani Mnamba wamesibitisha kutokea kubomoka kwa nyumba za Wananchi wakitupia lawama kwa Kiwanda cha Azam kuelekeza Maji ya Mvua katika mfereji uliopo kwa Wananchi, hata hivyo viongozi hao walienda kuonana na Utawala wa Kiwanda cha Azam na kusema wataita wataalam wakaguwe Maji hayo. Baada ya kuona kimya kwa muda. mrefu Wananchi wakiendelea kulalamika suala hili wamelipeleka ngazi ya juu Wilaya ya Mkuranga.  Mwandishi wa Mtandao huu waliamua kwenda Kiwandani Azam na kuonana na Arafat Mohamed HR amekili kupata malalamiko hayo kutoka kwa wananchi hata hivyo wanampango wa kuongea na Tanrood wabadilishe mtalo huo . hata hivyo amesema Maji ya Kiwandani hatoki nje kunamakalo makubwa yanayomiliki Maji ya Kiwanda hayo ni Maji ya Mvua yanayotililika kutoka katika Paa amesema suala hili litafikishwa kwa mmiliki wa Kiwanda Baresa hili liweze kufanyia kazi kwa kuwa Wananchi ndio majirani zao


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List