Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema amepokea msaada wa mifuko 600 ya cement,na ahadi ya Madawati MIA nne(400),kutoka kwa Shirika lisilo la kiserikali la SGM foundation yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 6 kwa ajili ya shule ya msingi Mbande. kwa lengo la kuongeza Madarasa na Ujenzi wa Uzio.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi ya shule ya msingi Mbande - Martin Jairo,amepokea na kushukuru kwa msaada huo. Pia amewataka Wazazi wafuatilie mwenendo wa watoto wao,ili wapate elimu iliyo bora itakayo changia katika maendeleo yao ya shule. pia amezungumzia suala la wanafunzi kujihusisha katika makundi hatarishi.
Mkuu wa Shule ya Mbande-Dauden mwakyambiki na Afisa elimu kata ya Chamazi-Balbina Ngalaba wameshukuru kwa msaada uliotolewa na kuwataka Wazazi, wanafunzi na Walimu kushirikiana ili kupata elimu iliyo bora.
TBN "TUNAISHUKURU WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI, ,SANAA NA MICHEZO ""
-
"Tanzania Bloggers Network TBN tunatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya
Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia ...
Saa 21 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni