Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Stephen Katemba ametoa wiki moja kwa watu wote wenye Mashamba Pori kuwasilisha Mpango kazi wa maeneo wanayomiliki, huku akiwataka wavamizi wa maeneo ya Serikali kuondoka mara moja kabla ya sheria kuchukua Mkondo wake. Aidha amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Watendaji kufanya kazi kwa uwadilifu na kutoa onyo kwa Watumishi hao kwa kuwataka kumaliza mgogoro ya ardhi ambayo idadi yake sasa inafikia 217. Mkurugenzi huyo amesema hatakuwa tayari kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 4 kwa ajili ya kununua eneo la Ujenzi wa Ofisi za Manispaa hiyo kwa kuwa yako maeneo yanayptosheleza Ujenzi huo, yaliyotengwa tangu enzi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere. Pia ameeleza mkakati wake wa kufufua Kisima Kikubwa kilichochimbwa enzi za Mwalimu Nyerere kilichokuwa na uwezo mkubwa wa kusambaza Maji safi na salama maeneo ya Kigamboni. Diwani wa Kata ya Somangila Kigamboni Frances Masanja Chichi pamoja na Viongozi wa mtaa wa Mbwamaji wamesema wapo tayari kushirikiana na Mkurugenzi huyo kutatua kero zilizopo ili waweze kuleta maendeleo. Zoezi la ukaguzi wa eneo lililopo mtaa Mbwamaji ambalo linalokusudiwa kujengwa Halmashauri ya Kigamboni, zoezi ambalo limeenda sambamba na Usafi wa Mazingira.
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
Saa 14 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni