ZIARA YA WAZIRI KAIRUKI YAIBUA MADUDU MRADI WAA TASAF

Waziri wa nchi ofisi ya rais na menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora mhe Anjella kairuki ametembelea mradi wa tasaf  mkoa wa dar es salaam na kubaini kuwa haujafanya vizuri kama serikali ilivyokusudia kuzisaidia kaya masikini sana.Akiwa wilaya ya temeke amesikitika sana kuona robo tatu ya wananchi waliopewa ni watu wenye uwezo na sio walengwa wa mradi,Pia kwenye ziara hiyo aliyofanya kata ya sandari na mtoni mtongani ambapo kwenye mkutano wa Hazara alisikiliza kero za wananchi na karibu wazee wote maskini sana waliouzulia mkutano huo wamesema hawajapata fedha hizo za mradi wa Tasafu.Waziri kairuki ametoa siku 30 kwa wale wote waliohusika na upotevu huo wa fedha warudishe wenyewe kabla ya sheria kuchukua mkondo wake. pia ametoa angalizo kwa watumishi wa tasaf kama endapo watashindwa kusimamia mradi huo,Serikali inaweza kuufuta mradi huo na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi hao. serikali haiwezi kuangalia fedha za mradi zikipotea bila ya kutimiza malengo yake.Watumishi hao wa tasaf wametakiwa wawajibike na kuwaingiza kwenye mradi wananchi ambao ni walengwa wa mradi Yaani kaya masikini sana. mwisho

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List