Watanzania wameshauriwa kujifunza kilimo cha ufugaji wa nguruwe ili kupata maendeleo ya kiuchumi.Hata hivyo wametakiwa waondokane na dhana potofu ya kusema nyama hiyo ina madhara ya kiafya kwa walaji wa mboga hiyo.Diwani wa kata ya vikindu ambaye pia ni mkurugenzi wa tandan formi od Nicholas John Kampa amesema inawezekana jiji la dar es salaam kuwa na upungufu wa nyama ya nguruwe kutokana na kuanguka paa la nyumba ya kufugia nguruwe wenye mimba katika shamba la tandan lililopo kata ya vikindu kijiji cha kisevule wilaya ya mkuranga mkoa wa pwani,Baada ya kuanguka kwa paa hiyo wamekufa nguruwe 25 wakiwa na ujauzito.Kampa amesema mkoa wa dar es salaam wanategemea nyama za kutoka shamba la tandan vikindu ambapo kwa siku ulisha tani 5 kwa siku.Wakati mkoa wa Dar es salaam unahitaji nyama tani kumi kwa siku. kutokana na kufa kwa nguruwe hao uzalishaji utashuka zaidi hivyo haitawezekana kupatikana hata tani tano ya Nyama.
BONDIA RAMADHANI MIGWENE AMUWEKEA MIKWALA ALBANO CLEMENT BAADA YA KUKIMBIWA
NA HABIBU PENGO
-
BONDIA RAMADHANI MIGWEDE baada ya kukimbiwa na mpinzani wake Habibu Pengo
aliesaini nae kuzipiga mara ya kwanza sasa amebadilishiwa mpinzani na
atache...
Miaka 2 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni