WAZAZI WAMETAKIWA KUTOWAFICHA WATOTO WENYE MGONGO WAZI NA VICHWA VIKUBWA BALI WAWAPELEKE HOSPITALINI.

Jamii imetakiwa kutowatenga au kuwanyanyapaa Watoto Wenye Mgongo wazi na wenye kichwa kikubwa bali wawapeleke Hospitali kupatiwa tiba ya magonjwa hayo.Kwa maelezo ya wataalamu kuna uwezekana mkubwa zaidi kupona kwa watoto wenye matatizo hayo sababu matibabu yake yapo na wengi wameshapona.  Wazazi wameshauriwa kuwapeleka mapema Hospiali watoto pinsi tu wanapogundua kuwa wana matatizo hayo ya kichwa kikubwa au Mgongo wazi,Hayo yamesemwa kwenye mkutano uliowakutanisha Madaktari,wazazi na wadau mbalimbali wa afya.Mkutano huo ulifanyika Hospitali ya Muhimbili Moi,Jijini Dar es salaam.DR SAMWEL SWAI mkurugenzi Moi amesema wazazi wajitokeze kuwapeleka Hospitali watoto wenye matatizo hayo ili wapatiwe tiba.DR LEMERI  MCHOME daktari bingwa wa magonjwa ya Mgongo wazi na kichwa kikubwa amesema wanakabiliwa na upungufu wa madawa na vifaha tiba.Wadau na wazazi wamesema wanapata usumbufu wa kukataliwa kukatiwa bima ya matababu kwa ajili ya watoto hao.Wameiomba serikali kuangalia njia ya kusaidia watoto hawa kupata bima ya afya kutokana na wazazi walio wengi kuwa ni watu wa kipato cha chini sana.Takwimu zinaonyesha
watoto wapatao elfu nne kila mwaka huzaliwa wakiwa na matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi lakini kati ya hao ni watoto mia tano tu ambao hufikishwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu. takwimu hizo zimetolewa na chama cha wazazi wenye watoto walio na matatizo hayo kwa kushirikiana na hospitali ya taifa ya muhimbili kitengo cha moi.Kitengo cha moi ambapo hutoa huduma hiyo kwa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi na hapa inabainishwa kuwa watoto wanaozaliwa na matatizo hayo ni wengi lakini takribani watoto 3500 hukosa matibabu kutokana na wazazi wao kutokuwa na elimu na hiyo,Hivyo huwapeleka kwa waganga wa kienyeji.Katika maadhimisho ya mtoto mwenye kichwa kikubwa duniani na mgongo wazi yanayofanyika kila oktoba 25.kwa TANZANIA hufanyika hospitali ya muhimbili kitengo cha moi jijini dar es salaam.Othman Kiloloma kaimu mkurugenzi mtendaji moi pia ni daktari bingwa wa upasuaji kichwa kikubwa na mgongo wazi ambaye anasema pamoja na utoaji wa matibabu hayo bure kwa mtoto chini ya miaka mitano bado wazazi na walezi wa watoto wanashindwa kuwapeleka hospitali na kuwaomba wazazi hao waachane dhana potovu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List