Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limawakata watu zaidi ya mia nne kupitia operesheni yake iliyoiendesha katikati na pembezoni mwa jiji hilo kutokana na kuhusika na makosa mbalimbali ya uhalifu. Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi,makosa hayo ni pamoja na yale ya kutumia silaha, unyanang'anyi wa kutumia nguvu, kununua na kupika pombe ya gongo ya sanjari na Wizi wa vifaa vya magari. Lakini licha ya umakini huo, changamoto hazikosekani kwa wahalifu kujaribu kulipima jeshi hilo na kisha kujikuta mikononi mwa Dola .Jeshi hilo, pia, kupitia kikosi cha kupambana na genge la wezi wa magari, limewatia nguvuni watu wawili, kwa kuhusika na Wizi wa magari manner yaliyoibiwa Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Kilimanjaro na Arusha. Pia jeshi hilo, Novemba 11 mwaka huu, katika maeneo ya Kinyerezi jijini Dar es salaam limefanikiwa kuwatia nguvuni watu watatu wakila njama za kutaka kuiba shilingi milioni mia mbili huku wakiwa na Bastola bandia.
UNAISHIWAJE PAWA KWA KUPANDA MLIMA LOLMALASIN ?
-
Wakati anamsifia mpenzi wake Msanii Mbosso aliimba “ _Kamusi namaliza
kurasa kukusifia”_ ,na akahitimisha kwa kusema anaishiwa pawa kwa kuwa
penzi la huyo...
Saa 2 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni