UVCCM WAMPONGEZA RAIS

Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (Uvccm)wilaya ya Ilala,wamempongeza Rais Dk John Magufuli kwa kutekeleza Ilani ya chama kwa kuwafichua na kudhibiti rushwa,ujangili sanjari na kujali wananchi wasio na uwezo kwa kufanikisha elimu bure.
Wakizungumzia kuunga mkono vita dhidi ya rushwa ndani ya chama hicho,vijana hao wameahidi kuwa vinara wa kuwafichua wote watakaohusika na tabia hiyo katika uchaguzi ujao wakidai wanataka kurudisha heshima ndani ya chama na kulinda maadili.

Mwenyekiti wa Uvccm,Ndugu Alfred Tukiko na katibu CCM Wilaya ya Ilala Kafuge Joel wamempongeza Rais Magufuli kwa kurudisha uadilifu na nidhamu ndani ya CCM na kuahidi kutoa ushirikiano kwa kusaidia chama kutekeleza Irani yake.
Katika mkutano huo Uvccm kupitia serikali yake imetangaza vita dhidi ya watu wenye nia ya kurudisha nyuma jitihada za kuleta maendeleo na wanaotishia uvunjifu wa AMANI.

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List