KIFO CHA MUNGAI

Aliyewahi kuwa Waziri katika wizara tofauti na Mbunge wa jimbo la mafundi kaskazini kwa miaka 35,Joseph Mungai anatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja karimjee jijini Dar es salaam. Msemaji wa familia ambaye ni mtoto wa tatu wa Marehemu,William Mungai amesema kutoakana na Baba yake kushika nafasi mbalimbali Serikalini,familia wameona pia ni muhimu kwa wale wanaomfahamu kushiriki tukio hill kabla ya kusafirishwa. Marehemu Mungai alifikwa na mauti jumanne Saa kumi jioni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa tumbo. Nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam ,Viongozi na wananchi wamefika kwa ajili ya kutoa pole na ndipo Waziri wa Nyumba,maendeleo ya Makazi,William Lukuvi anamzunguzia marehemu Mungai.Naye Mbunge wa zamani wa jimbo la sumbawanga,Crisanti Mzindakaya pamoja na mwenyeketi wa serikali ya Mtaa wa Osterbay, Zefrin Lubuva wakawa na haya ya kusema juu ya marehemu.

vox:i: Cristant Mzindakaya - Mbunge wa zamani wa sumbawanga  :ii :Zefrin lubuva -Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Osterbay .Joseph Mungai alizaliwa mwaka 1943 na kusomea masuala ya uchumi na utawala sanjari na kushika nyazifa mbalimbali ndani ya serikali na chama .                

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List