Mwili wa Spika Mstaafu wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania marehemu Samuel Sitta aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia jana jijini Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu unatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi wiki hii.
Msemaji wa familia Gerald Mongela ameiambia Channel Ten kuwa mara baada ya mwili huo kuwasili utapelekwa nyumbani kwa marehemu Masaki kwa ajili ya maandalizi ya kuagwa ambapo kwa mujibu wa familia hiyo heshima za mwisho zitatolewa katika viwanja vya Karimjee siku ya Ijumaa na baadae kusafirishwa kuelekea mkoani Dodoma ambapo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watapata nafasi ya kuaga kabla ya mwili kusafirishwa kuelekea Urambo Mkoani Tabora kwa ajili ya maziko.
Baadhi ya watu waliowahi kufanya kazi kwa karibu na Marehemu Samuel Sitta wameelezea wanavyomkumbuka hususan katika utendaji wake wa kazi
TUFANIKISHE PAMOJA YAWAKUMBUKA WATOTO YATIMA TEMEKE
-
Kikundi cha Kijamii cha TUFANIKISHE PAMOJA kimeungana na Uongozi wa Kituo
Cha Kulelea Watoto yatima na wenye uhitaji cha Valentine Home Centre
kilichopo...
Saa 21 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni