KATIBU WA KIJIJI ATIMULIWA.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani  MAJID HEMED amemvua madaraka KATIBU wa kitongoji cha Pingu kata ya Pela Hamisi Malifedha kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za maendeleo.

Baada ya kumvua madaraka katibu wa kitongoji cha Pingu,Mkuu wa WILAYA huyo amemtaka Mwenyekiti wa kitongaji hicho Miraji Said Dibwe awasilishe taarifa za mali zake ndani ya saa nane na asifanye kazi yoyote ndani ya siku 14 mpaka atakapotoa maamuzi.

Tuhuma zinazowakabili viongozi hao wa kitongoji cha Pingu ni ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa Zahati ambapo serikali ilitoa milioni 60 tangu mwaka 2011 lakini mpaka leo haijakamilika.
Ubadilifu mwengine uliobainika ni fedha za ujenzi wa darasa moja lililojengwa kwa shilingi milioni 14,ambapo kwa mujibu wa tathimini ya majengo darasa hilo halilingani na gharama hizo.
Baadhi ya wananchi wakitoa kilio chao kwa mkuu wa wilaya huyo wamelalamikia mgogoro wa wakulima na wafugaji.
Tedd Sanga Mratibu Mkuu Ekwa Vicoba ametoa ushauri kws serikali itenge matumizi bora ya ardhi ili kutatua migogoro inayojitokeza mara kwa mara.
Hata Hivyo wananchi wamemuomba Mkuu wa wilaya huyo kuwasaidia kutatua mgogoro huo wa ardhi Na kumshukuru kwa hatua alizochukua.

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List