Tanzania Bara yaadhimisha miaka 55 ya Uhuru

Rais wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Magufuli leo amewaongoza watanzania katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara, uliopatikana Desemba 9, 1961.Sherehe za maadhimisho hayo zimefanyika katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam na kuhudhuria na maelefu ya watanzania, chini ya mgeni rasmi Rais Magufuli.
Katika sherehe hizo ambazo ni za kwanza tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya tano, Rais Magufuli amewasili na kupanda gari maalum alipokuwa akiwasalimia wananchi, kisha kupigiwa mizinga 21 na baadaye kukagua gwaride la heshima.
Rais Magufuli pia amepata fursa ya kushuhudia maonesho mbalimbali ya ukakamavu kutoka kwa vikosi mbalimbali vya majeshi ya ulinzi, ikiwemo maonesho kutoka kwa vikosi vya makomando.
Pia vikosi hivyo vimepita mbele ya mgeni rasmi kutoa heshima na kwa mara ya kwanza watanzania wameshuhudia gwaride la kimyakimya katika sherehe za uhuru ambazo mwaka jana zilifutwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa watanzania kufanya usafi pamoja na kuokoa gharama.

Kaulimbiu ya sherehe hizo kwa mwaka huu ni: Tuunge mkono jitihada za kupinga rushwa na ufisadi na tuimarishe uchumi wa viwanda kwa maendeleo yetu.
Baadhi ya watu waliokosa nafasi ndani ya Uwanja wa Uhuru na kuamua kutafuta nafasi katika ngazi za uwanja wa taifa ili kushuhudia kinachojiri Uwanjani.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List