Rais Magufuli akutana na Rebecca Garang

Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini, Rebecca Nyandeng Garang de Mabior.
Baada ya mazungumzo hayo,Mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Mabior, amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania kuonana na Rais Dkt Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya afrika ya Mashariki kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan ya Kusini.
Amemuomba Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake wa jumuia ya Afrika ya Mashariki kulisaidia Taifa la Sudan ya Kusini kutafuta suluhisho la mgogoro unaolikabili taifa hilo na kurejesha amani.
"Tumefarijika kuwa hapa katika ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dkt Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuia ya Afrika ya Mashariki, akishirikiana na viongozi wenzake wa jumuia hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia ili Taifa la Sudan ya Kusini liwe Taifa lenye amani, hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa tunachokitaka ni Amani katika nchi yetu na hiki ndicho kilio chetu"
Rais Magufuli kwa upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan ya Kusini kutafuta njia muafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa hilo.
"Mama Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi ya Sudani ya Kusini hivyo, ningezisihi pande zote zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la Sudani ya Kusini"

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List