Jumuiya ya wanawake CCM(UWT),Wamempongeza Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa mabadiriko aliyofanya ndani ya chama cha mapinduzi na mfumo wa serikali kwa ujumla.Pamoja na kuwapa pongezi wateule wapya wa sekretarieti ya Halmashauri kuu Taifa.
Pongezi hizo ni dhidi ya mageuzi na mabadiriko makubwa yaliyofanywa na Mwenyekiti wa Chama na Rais wa Tanzania ikiwamo,Kupunguza idadi ya wajumbe na viongozi wasiokuwa na ulazima sana.
Mwenyekiti wa UWT Janneth Masaburi amempongeza sana Mh Rais na Mwenyekiti wa CCM kwa kunukuu usemi wa Mwal.Julias Kambarage Nyerere "heri kuwa na jeshi dogo lenye nidhamu kuliko jeshi kubwa lisilo na nidhamu.Pia amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi kujituma katika shughuli za jamii na kumsaidia Rais katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Viongozi hao kwa umoja wao wamesema watashirikiana kwa karibu na Mwenyekiti Dkt John Pombe Magufuli kwa kuzingatia maslai mapana ya Taifa na kuwajibika ili kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya Tano.
TARURA MKOA WA DAR KUBORESHA BARABARA
-
Na Shushu Joel, Dar.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga ameeleza
mikakati ya uboreshaji wamiundombinu ya Barabara katika j...
Siku 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni