VIKOBA WAOMBWA KUWAKUMBUKA WATU WENYE MAZINGIRA MAGUMU

Wanavikundi vya kuweka na kukopa(Vikoba) wa maeneo ya Zingiziwa Chanika wametakiwa kuwakumbuka watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu sanjari na wajane baada ya kupata gawio zao.
Wito huo umetolewa wakati wa kikundi cha MFANO BORA kugawana faida walizojiwekea kwa miaka miwili ya milioni 39 na kuamua kuitoa kwa watu wanye mahitaji maalumu ikiwemo Chakula,mavazi na vifaa kwa watoto wa shule.
Hussein Wambura Togoro ni Diwani wa Kata ya Zingiziwa ambaye ambao anawakumbusha wananchi wengine zaidi kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa ili wanufaike kiuchumi kwa kufuga samaki,Kuku na mifugo mingineyo  sambamba na kupata mafunzo ya nidhamu ya fedha.
Naye Mchungaji Alex Erasto Mwanga wa kanisa la KKT chanika ameitaka jamii nchini kuwajali watu wenye mahitaji maalumu na kuwapatia misaada inayostahili kutokana na mazingira magumu waliyokuwa nayo ikiwemo kukosa chakula.
Baadhi ya viongozi wa kikundi cha MFANO BORA wamesema wanajisikia raha kuona binadamu wanaishi kwa Amani na Upendo.

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List