Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imesema haihusiki na utoaji wa ajira za walimu nchini.

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imesema haihusiki na utoaji wa ajira za walimu nchini, isipokuwa inachokifanya ni uhakiki wa taarifa za walimu wenye sifa za kuajiriwa serikalini.Hatuhusiki na ajira za walimu - Wizara ya Elimu
Mhandisi Stella Manyanya
Akizungumza na EATV leo, Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa kwa sasa wizara hiyo inapitia taarifa (CV) za walimu waliohitimu ngazi ya Stashada na Stashahada, na baada ya hapo itazituma taarifa hizo katika Wizara ya Utumishi ambao ndiyo wanaohusika na kuajiri.
Akizungumzia sababu za kuwatenga wahitimu wa ngazi ya cheti, Manyanya amesema uhitaji mkubwa uliopo kwa sasa ni kwa walimu wa sekondari hususani wa masomo ya Phisics, Hisabati, Chemistry na Biolojia, hivyo inawahitaji kwa haraka zaidi walimu hao huku akisema wahitimu wengine ambao siyo wa masomo hayo na ambao siyo kwa ajili ya kufundisha sekondari, wasubiri utaratibu wa wizara inayohusika na utumishi.
"Siyo kwamba hatuhitaji walimu wa shule za msingi, lakini uhitaji mkubwa tulionao kwa sasa ni walimu wa sekondari, sisi hatuajiri, sisi tunafanya uhakiki, na sasa tunapitia CV za wahitimu waliotuma taarifa zao, tukishajiridhisha na wale ambao taarifa zao ni sahihi na wana sifa tunazohitaji, tunazipeleka Utumishi, hao ndiyo wataajiri, halafu majina yatapelekwa TAMISEMI kwa ajili ya kupangiwa maeneo ya kazi" Amesema Manyanya
Kuhusu idadi ya walimu wanaohitajika haraka, Manyanya amesema, wanahitajika walimu wengi kuliko idadi waliyoitoa mwanzo, na kuwataka wote waliotuma taarifa zao wawe na subira kwa kuwa mchako wa uhakiki bado unaendelea na majina yatatangazwa muda mfupi ujao ambao hautazidi kipindi cha miezi mitatu.
  

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List