MZEE KINGUNGE AELEZA KWANINI WAPINZANI HAWATASHINDA 2020 KWA HALI HII

Wakati ambapo Chadema imekuwa ikidai kuwa na uhakika wa kushinda uchaguzi mkuu ujao (2020), mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru amewatahadharisha kuhusu vikwazo viwili vitakavyowazuia.
Akizungumza jana katika mkutano na vijana wa Chadema waliokamatwa mwaka jana katika uchaguzi mkuu kwa tuhuma za kuingilia zoezi la kuhesabu na kutangaza matokeo ya urais, walioachiwa huru wiki hii, Mzee Kingunge alidai kuwa wapinzani wasahau kuingia Ikulu kama hakutakuwa na Tume huru ya uchaguzi pamoja na Katiba Mpya.
“Yako mambo ambayo inabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni Tume Huru ya Uchaguzi. Suala hili lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo, sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” Mzee Kingunge anakaririwa.
Aliongeza kuwa Katiba Mpya inapaswa kudaiwa ili kuondoa kipengele kilichoko kwenye sheria ya sasa kinachopinga matokeo ya rais kuhojiwa mahakamani. Alisitiza kuwa ili kufanikiwa katika hilo inahitajika nguvu ya pamoja ya kudai mambo hayo kwa watawala.
Katika hatua nyingine, Mzee Kingunga aliwapa pole na kuwapongeza vijana hao akiwatia nguvu kuwa hata wakati aliposhiriki harakati za kudai uhuru chini ya Tanu haikuwa rahisi na kwamba walijitolea na kuweka kando hata mishahara mikubwa.
“Ninyi mnapambana katika mazingira magumu, na wazee wenu pia tulipambana hivyo,” alisema.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ambaye alieleza kufurahi kuwaona vijana hao na kuwaeleza kuwa ‘yaliyopita si ndwele, wagange yaliyopo na yajayo’ kwani bado inahitajika nguvu kubwa zaidi hasa ya vijana.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List