KIKWAZO CHA USHINDI WA MAGUFULI 2020.

Wananchi wameshauri serikali ya awamu ya tano kutimiza ahadi zao bila kupindisha pindisha.Haya yamesemwa wakati uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa kwa kiwango cha asilimia sita.
Wananchi wamedai kukosa kwa ajira za wahitimu wa shahada na stashahada za ualimu kumepunguza mvuto kwa rais huyo kutokana na kuwa hilo ni kundi kubwa la wasomi na wenye ushawishi katika jamii yao.
Pili ukilinganisha na miaka iliyopita ya awamu za maraisi wengine safari hii wanafunzi wengi wa elimu ya juu wamekosa mikopo na waliopata wamepata kwa kiasi kidogo hivyo wengi kushindwa kuendelea na masomo kitu ambacho wao na jamii zao wameonekana kuchukia sana na kuona utawala wa Awamu ya Tano kama utawala usiofaa.
Kutopanda madaraja na Mshaala ni kikwazo kingine cha Rais Magufuli kufanya vizuri 2020.Hili linaambatana na uhaba wa ajira ambao umekuwa kwa zaidi ya asilimia nane ukilinganisha na Utawala uliopita.
Kushuka kwa elimu na utoaji wa huduma za jamii hususan upotevu mkubwa wa dawa hospitalini.
Kuongezeka kwa matukio ya kutisha ya uhalifu,makundi ya wezi watoto(panya road),ukabaji na ujambazi.
Cha kushangaza richa ya juhudi kubwa kuzuia rushwa lakini inaonekana kushika kasi kubwa na kutawala ofisi nyingi za serikali hivyo Rais Magufuli anatumia muda mwingi kutengua viongozi hao.
Maisha yanazidi kuwa Magumu kwa Wananchi na kipato kushuka hata Milo (diet)kubadilika.Inakadiliwa watanzania wanakula milo miwili kwa siku na mlo mmoja Tu kwa idadi kubwa ukilinganisha na wanaokula Milo mitatu.
Matamko ya viongozi ambayo yamekuwa yakipishana na kuonekana wanasema mambo wasiyokuwa na uhakika nayo.
Mwisho Wananchi wamemuomba Mh.Rais Dkt John Pombe Magufuli kuangalia hizo changamoto na kuzifanyia ufumbuzi mapema ili kujihakikishia ushindi 2020 .

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List