MWAKA MPYA NA CHALINZE MPYA.

Mbunge wa JIMBO la chalinze Mkoani pwani Mhe Ridhiwani kikwete anatarajia kufanya ziara katika JIMBO hilo kutatua kero za Wananchi ikiwemo shida ya Maji,sanjali na kutafuta suluhu ya Migogoro ya wafugaji na wakulima.


Akiongea na Mwandishi wa blog hii Mhe Ridhiwani Kikwete ameonyesha malengo thabiti ya kuwasaidia Wananchi wa chalinze kwa kuhakikisha anatatua kila kero sugu,haya yameonekana katika vipaumbele vyake vya mwaka 2017 ikiwemo ziara ya kutathimini maendeleo ya chalinze kwa ujumla.

Pia mbunge Ridhiwani amewataka wananchi wa chalinze kujikita katika kilimo cha matunda kwa sababu ya kuwahi fursa kwa mwekezaji ambaye ndani ya mwaka huu atafungua kiwanda cha kuchakata matunda katika kijiji cha mboga.Mhe Ridhiwani Kikwete amesema kwa mwaka huu ni vyema wananchi wakafanya kilimo chenye tija kwasababu kutakuwa na fursa kubwa kutoka katika viwanda na hivyo watakuza kipato chao na uchumi wa chalinze.
Akizungumzia suala la madini amesema wanazidi kubuni njia ili kuongeza pato linalotokana na madini na kuwanufaisha wanachalinze Kwa ukubwa zaidi japo kwa sasa limekuwa lakini bado halijafikia lengo ambalo limekusudiwa.
Mwisho Amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi katika mikutano yake ili kutoa kero zote zinazo wakabili zipatiwe ufumbuzi.
Hayo yamesemwa katika sherehe za kukaribisha mwaka mpya zilizofanyika chalinze kijijini Msoga.

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List