BUSARA YA RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE INAVYOISHI NDANI YA RIDHIWAN KIKWETE MBUNGE WA CHARINZE.

Mbunge Ridhiwan Kikwete amekuwa Mbunge wa Mfano wa kuigwa kwa wabunge Vijana kutokana na kutumia muda mwingi katika shuguli za maendeleo za kufanya Chalinze kuwa sehemu bora na jimbo lenye maendeleo zaidi Tanzania.Tofauti na wabunge wengi Vijana ambao wamekuwa wakirushiana Vijembe na Maneno katika mitandao ya Jamii na hata Bungeni na kusahau ahadi na matatizo ya wananchi wao.Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete anatumia muda mwingi kuelezea ni nini atafanya na anafanya nini kwa ajili ya Wananchi wa jimbo la lake la Chalinze.

Nilipopata bahati ya kuonana naye na kufanya mahojiano nikagundua kwa kiasi kikubwa anaishi na busara za Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete sababu alikuwa anajibu maswali kwa kuonyesha mwelekeo wa kazi zake za ubunge akiweka vipaumbele vya Maji,Miundombinu,na Viwanda vipya vitakavyoanza kazi mda sio mrefu ambavyo vitawasaidia wanachalinze kukuza kilimo na kipato chao,Mbali na hapo akazungumzia sana kuhusu kilimo na utani wa kawaida kwa mbali kama ilivyo kwa baba yake.Licha ya kumpa nafasi ya mara kwa mara hakuweza kutoa jibu la kijembe,kumsema mbunge au kujibu majibu ambayo hayamo katika mpango wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo za jimbo la Chalinze.

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete ni raisi aliyeiongoza Tanzania kwa mafanikio huku akichukua tuzo na medani mbalimbali za kitaifa na kimataifa na kufanikiwa kumkabidhi kijiti Dkt John Pombe Magufuli.Sifa ya Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ni upole wa kutojibu vijembe wala kashfa zaidi kuongeza utendaji kazi wake ila kuipa hadhi na heshima nchi.Wakati akiwa Rais alikumbana na upepo mzito wa siasa ya vyama vingi ambapo alipambana na kuleta maendeleo na Matunda yake ni ushindi wa CCM na Imani ya Watanzania kwa chama hicho cha mapinduzi.
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amekuwa akisisitiza siasa sio vita,Upendo na Maendeleo ya kweli kwa watanzania na Kwa Sasa Tunaona Mh:Rais Dkt John Pombe Magufuli anasema maendeleo hayana Chama na kuwapa nafasi wabunge wa upinzani kila sehemu anapotembelea hizo ni jitihada za Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika kudumisha upendo na amani kwa watanzania.

Karibuni Vyombo vya habari na watu kwenye mitandao ya jamii wamekuwa wakimwandama Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete katika mambo mbalimbali lakini hakujibu hata moja na zaidi alikuwa anajituma katika shughuli za maendeleo chalinze na hata alipojibu alijibu majibu mafupi ya mzaha au utani fulani na ya kufurahisha kama ilivyokuwa kawaida kwa Baba yake Rais Mstaafu wa Tanzania.

Wanasiasa wa kipindi hiki wana mengi ya kujifunza toka uongozi wa Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mbunge wa Chalinze sababu wao kipaumbele ni maendeleo ya watanzania na maneno hayana nafasi kabisa kwao(Wacha Maneno weka mziki)

Imeandaliwa na Stuart George

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List