Muuguzi mstaafu wa hospitali ya Mwananyala ambaye alitumikia kwa zaidi ya miaka 30.Bi Victoria Makala Mkenso (maarufu kama Bibi Kanitangaze au Kanisambaze) amefanya sherehe kubwa Nyumbani kwake baada ya kulipwa mafao yake ya kiinua mgongo na kusherekea na majirani,rafiki na ndugu.Pia ameweza kumshukuru mwenyezi MUNGU kwa kumfikisha hapa na kustaafu salama bila dosali yoyote kazini.Pia amewataka wauguzi wafanye kazi kwa wito na kutojali maslai yao binafsi,kwa kuwa kazi ya kuwahudumia wagonjwa inahitaji uwe na moyo wa uzalendo na kujitolea.Pia amekemea swala la rushwa kwa kuwaomba wauguzi na wahudumu kutoomba wala kupokea rushwa sababu ni adui wa haki na maendeleo.Mwisho alielezea mafanikio aliyoyapata kutokana na kazi yake kama kuwa na nyumba,Kisima cha maji na gari ya kutembelea.
BALOZI MUSSA AKAGUA MAJENGO YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI.
-
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya miradi ya Wizara, Balozi Said Shaib ...
Saa 2 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni