Jeshi la polisi wilaya ya bagamoyo mkoa wa Pwani limedaiwa kuwaua Vijana wawili wa familia moja ya jamii ya wafugaji.Vijana hao wameuwawa na askali polisi wa wilaya ya BAGAMOYO katika kijiji cha Kidomlole kata ya Fukayosi mkoani PWANI baada ya kuhitaji kuhesabu mifugo yao ambayo askari hao walitaka kuichukuwa bila kuhesabiwa kwa kile kinachodaiwa ni zoezi la kuwaondoa wafugaji walioingia wilayani humo kinyume na taratibu.
Baadhi ya wafugaji wakizungumza baada ya uongozi wa chama cha wafugaji tanzania na jeshi la polisi kufika katika eneo hilo wameeleza,
MELIKUTA KAMBALELEGA akielezea jinsi hali ilivyotokea na kupata majeruhi. Huku YOHANA ROGER na baba mzazi wa watoto hao kambalelega Gisamoda walielezea pia hali ya tukio zima lilivyokuwa.
Hata hivyo baada ya kutokea mauji hayo mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu jamii hiyo yawafugaji ilipiga kambi katika eneo hilo yalipofanyika mauaji na kudai kutokukubali kuondoa miili ya vijana hao kuifadhiwa lakini jitihada za kiongozi wa chama cha wafugaji Tanzania BWANA MAGEMBE MAKOYE na Wazee wa kimila wa eneo hili wakatumia busara kuwaomba wafugaji hao kuwa wavumilifu huku taratibu zikifuata ili kuwachukulia hatua waliofanya tukio hilo.
Alhaj MAJID MWANGA ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo na mwenyeiti wa kamati ya ulizi na usalama ya wilaya hiyo je anazungumziaje tukio hilo?
Ni miezi 6 sasa tangu kutokea kwa mauji ya mmoja wawafugaji katika kijiji cha makurunge na hili ni tukio llingine ambao limedaiwa kufanya na askari polisi wa wilaya hiyo hata hivyo miili ya vijana hao imechukuliwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi imehifadhiwa katika hosptali ya wilaya bagamoyo kwa uchunguzi zaidi na walifariki SAINGA KAMBALELEGA na LUMAYE KAMALELEGA.
BALOZI MUSSA AKAGUA MAJENGO YA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MALAWI.
-
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya miradi ya Wizara, Balozi Said Shaib ...
Saa 17 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni