JPM AMTEUA MAMA SALMA KIKWETE, KUTINGA BUNGENI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo amemteua Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Taarifa za uteuzi huo wa Mama Salma ambaye ni mke wa aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, zimetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mama Salma ataapishwa hivi karibuni kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati akiwa ‘First Lady’, Mama Salma aliwekeza nguvu zake katika kusaidia juhudi za kuwakwamua wasichana na wanawake kwa ujumla katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwa ni pamoja na afya na uchumi.
Mama Salma pia alionesha uwezo mkubwa wa kisiasa hasa wakati wa kampeni mbalimbali za kisiasa, ambapo alikinadi vyema Chama Cha Mapinduzi.

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List