RC MAKONDA ; NIMARUFUKU KUUZA CD BILA KIBALI,AU KITAMBULISHO KATIKA MKOA WA DSM, ATAJA MAJINA 13 YA VINARA NA KUAMURU WARIPOTI POLISI CENTRAL IJUMAA


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam  Mhe.Paul Makonda amewataka wote wanaofanya biasha ya kuuza CD na DVD kwa kutembeza mtaani  mkononi pamoja na wanaodurufu kazi za   wasanii kuacha  maramoja kabla hawaja chukuliwa hatua za kisheria .

 

Akizungumza katika maandamano ambayo yaliratibiwa na wasanii wa filamu na na kuhusisha ofisi ya mkuu wa mkoa na Wizara ya Habari utamadun sanaa na Michezo yaliyo anzia Ilala boma hadi karikariakoo Mhe Makonda amekemea vitendo hivyo na kumtaka kila anayetaka kuuza filamu za nje kuwa navitambulisho maalumu vinavyotolewa na wizara husika .

 

Aidha  amewataja  majina ya watu 13 nakuwataka waripoti  Polisi kituo cha kati siku ya ijumaa kwa ajiri ya mahojiano maalumu  kuhusiana na matumizi ya mitambo ya kudurufu  filamu na amepiga marufuku uuzajiwa filamu za ngono jijini   Dar es salaam kwa kuwa ziko kinyume na maadili ya Mtanzania.

 

Amewataka wasanii kufurahia jasho lao kwani wanafanya kazi ya ziada katika kutekeleza kazi zao na kuanzia leo wasanii hao wataanza kunufaika nazo kwani sheria kali na utekelezaji utafuatwa.

 

Moja ya madai ya  wasanii hao ni uuzaji wa filamu za nje ambazo huuzwa kwa gharama ya chini  kuanzia 700 kwa bei ya jumla hadi 1000 rejareja  huku filamu za nyumbani zikiuzwa kwa bei ya juu kutokana na kodi na gharama nyingine wanazotozwa wasanii hao.


Kwa mujibu wa sheria ya filamu ya  1979 inamtaka muuzaji wa filamu za nje na ndani kufuata utaratibu maalum na akitaka  kuingiza filamu yoyote lazima ajaze  form ya kuomba  kazi hiyo.

Kwa upande wa wafanyabishara hao mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Salim Majonjo, wamedai wanapata wakati mgumu kuuza kazi za wasanii wa Bongo Movie kwa madai hazina ubora na zinazungumzia mapenzi ndiyo maana ameamua kugeukia kwenye soko la filamu nje.

“Mhe. Mkuu wa mkoa utufikirie na sisi wafanyabiashara  wadogo, sisi ndo tunajua hali ya soko la filamu likoje, ni filamu chache za Bongo ambazo unaweza ukauza tena zinahesabika. Yaani unaweza kukaa toka asubuhi mpaka jioni na usiuze filamu hata moja lakini filamu za nje zikawa zinatembea muda wote, stori zao kila siku ni zile zile watu wanachoka. Lakini ukileta filamu ya marehemu Kanumba inauza tena sana kwanini wao filamu zao haziuzi. Mimi ningewashauri wafanye kazi nzuri ambazo zitawavutia mashabiki wao huo ndio utakuwa muarobani wa hicho wanachokizungumzia,”alisema .

Rado, ni mmoja kati ya wasanii wa filamu ambao walikuwa katika opereshini hiyo,  yeye ameishukuru ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa hatua hiyo huku akiwataka Watanzania kwa jumla kuwaunga mkono.

“Kwanza nakushukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa hatua hii nzuri, sisi kama wasanii tunatambua juhudi za serikali katika kuhakikisha wasanii wananufaika na kazi zao pia serikali inapata kodi yake. Sisi kila msanii analipa kodi kupitia movies zetu, kila movies ikiuzwa asilimia 30 inaenda kwa serikali kwa hiyo mnaona ni namna gani tunalipa kodi. Kwa hiyo sisi tunataka na hawa ambao wanaingiza filamu za nje walipe kodi kama sisi kwa sabubu wote tunatumia soko moja tena mbaya zaidi wao filamu zao wanauza kwa bei ya chini zaidi,” alisema .

Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akizungua  katika mkutano huo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda katikati akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bi. Bi. Joyce Fissoo wakati akizungumza katika mkutano huo.

Kamanda Wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Simon Sirro akizungumza katika mkutano huo ambapo ameonya wale wote wanaouza filamu za Ngono na za kigaidi amesema hao watapambana na mkono wa dola.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List