Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameagiza vituo vya redio na runinga nchini kusoma vichwa vya habari tu vya magazeti kuanzia kesho.
Dk. Mwakyembe ameyasema hayo leo alipokuwa akitoa ‘neno’ kama mgeni rasmi katika maadhimisho hayo jijini Mwanza. Amesema kuwa kwa kusoma vichwa vya habari tu, wananchi watakuwa na hamu ya kutaka kuyasoma magazeti kupata habari kamili. Hivyo, watanunua.
Waziri Mwakyembe pia amewahakikishia waandishi wa habari kuwa Serikali itaendelea kulinda haki na uhuru wa vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na kutoa ulinzi kwa waandishi wa habari za uchunguzi.
Katika hatua nyingine, ameahidi kuwa wizara yake kupitia Idara ya Habari Maelezo itahakikisha waandishi wa habari wanapewa ushirikiano wa kutosha wanapohitaji taarifa kutoka Serikalini.
Amesema kuwa wizara yake itaweka utaratibu wa kukutana na waandishi wa habari kila mwezi ili kujadili changamoto wanazopitia katika kupata habari kutoka kwa vyanzo vya Serikali.
DKT. DORIYE AVISHWA CHEO KUAPISHWA KUWA KAMISHNA WA UHIFADHI NCAA.
-
*Na Kassim Nyaki, Karatu.*
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb) kwa niaba
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Sa...
Dakika 9 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni