DIAMOND PLATINUMZ KAWATENGENEZEA WA TANZANIA MARASHI KWA BEI NAFUU

Diamond kuwapa Watanzania ‘kitu’ kwa shilingi 300
Baada ya kuingiza sokoni marashi ya ‘Chibu’ kwa shilingi laki moja na nusu, Diamond ameamua kuwapa Watanzania bidhaa ya bei wanayoimudu ya shilingi 300.
Akifunguka jana kupitia The Playlist ya 100.5 Times Fm, Diamond alisema kuwa anaendelea kuunga mkono sera ya Rais John Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kwamba wiki hii ataingiza sokoni bidhaa yake hiyo ili kila Mtanzania aweze kuimudu.
“Inaweza kuwa Jumatano… tutaingiza sokoni bidhaa nyingine kwa shilingi 300 tu, hii najua kila Mtanzania ataimudu. Sasa kama mtu atashindwa kununua cha shilingi 300, labda sasa utakuwa unataka bure,” Alisema Chibu Dangote.
Naye meneja wake, Salaam alieleza kuwa Diamond hivi sasa ni kiwanda na ataendelea kufanya muziki huku akiingiza sokoni pia bidhaa mbalimbali.
Angalia hapa sehemu ya mahojiano yake:

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List