Taifa Stars yaonyesha makali Cosafa, Kichuya akifunga mabao mawili
Mshambuliaji Shiza Kichuya jana alikuwa nyota wa mchezo baada ya kuifungia Taifa Stars mabao mawili katika mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Cosafa dhidi Malawi nchini Afrika Kusini.
Kichuya alifunga mabao hayo katika dakika ya 13 na 18 huku akitunukiwa zawadi ya mchezaji bora wa mechi hiyo iliyomalizika kwa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kichuya alifunga bao la kwanza akimalizia krosi ya Saimon Msuva wakati bao lake la pili lilitokana na shuti kali alilopiga, akimalizia pasi ya Elias Maguli.
Baada ya ushindi huo, Stars itakabiliana na Angola katika mchezo unaofuata kwenye Kundi A ambao utafanyika Juni 27.
MLOGANZILA YATOA UVIMBE KWENYE MAPAFU KWA KUTUMIA MATUNDU MADOGO
-
Mloganzila yatoa uvimbe kwenye pafu kwa kutumia matundu madogo
Kwa mara ya kwanza wataalam wazawa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila
wamefanya upa...
Saa 15 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni