Vanessa Mdee afunguka kuhusu kupigana chini na Jux
Wale ndege tetere, Vanessa Mdee na Jux waliokuwa wakiruka pamoja kwa mahaba, sasa ni rasmi hawako pamoja tena.
Vee Money amethitisha utengano huo alipofanya mahojiano na kituo cha redio cha Soundcity nchini Nigeria. Alisema kuwa hivi sasa kila mmoja anaendelea na maisha yake.
“Mimi na Jux tulikuwa… ila sio tena na kila mtu ameendelea na maisha yake,” alisema Vanessa.
“Kulikuwa na mambo mengi yaliyokuwa yanaendelea kati yetu, lakini ninafurahi kuwa tumeyapita na kila mmoja amefanikiwa. Yeye [Jux] amefanikiwa na alikuwa na wimbo mpya,” aliongeza.
Wiki hii, Vanessa alikuwa mmoja kati ya watu waliompongeza Jux kwa kuhitimu shahada yake ya masomo ya TEHAMA nchini China. Hivi sasa wanaitana, ‘dada na kaka’.
Wawili hao walianza uhusiano wa mapenzi kwa siri mwaka 2013, kabla ya kuweka mambo hadharani mwaka 2014. Jux aliuweka moyo wake kwa Vannessa baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Jackie Cliff kufungwa jela nchini China kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya.
CRDB BANK YAZIDI KUIPAISHA KILI MARATHON
-
Hafla ya msimu wa 35 wa mbio za Kili Marathon imefanyika leo katika viwanja
vya ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo benki ya CRDB imeendeleza
udhami...
Dakika 11 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni