MBUNGE WA CHALINZE ASHIRIKI ZIARA YA RAISI CHALINZE

Mbunge wa Chalinze ameshiriki kwenye Ziara ya Mheshimiwa Raisi Dr.John Magufuli alipofika Wilaya ya Bagamoyo.

Ziara hiyo ya Raisi ambayo ilikuwa na kazi ya Kufungua Miradi ilianza na ufunguzi wa Kiwanda kikubwa cha matunda cha Sayona kilichopo Mboga Wilaya ya Chalinze. Pamoja na kumkaribisha Mheshimiwa Mbunge alimuhakikishia Mheshimiwa Raisi juu ya KUMUUNGA mkono katika hatua anazochukua ikiwemo kupambana na Ufisadi na kuwahakikishia Watanzania kutawala Uchumi wao. Mheshimiwa Mbunge alimueleza juu ya jitihada ambazo Wana chalinze wanazifanya kujikomboa katika Uchumi tegemezi.

Mheshimiwa Mbunge alimueleza Mh.Raisi jinsi Halmashauri yao ilivyofanikiwa kukusanya fedha kwa kuvuka kiwango cha makusanyo. " Mh. Raisi halmashauri yako hii ya Chalinze imefanikiwa kukusanya zaidi ya Asilimia 102 juu ya makadirio mbayo tulikuwa tumejipangia. Fedha hizi zitapelekwa katika miradi ambayo inagusa wananchi wa chini kabisa ikiwemo kuimarisha huduma za afya, maendeleo ya jamii, mikopo kwa wakina mama na vijana na pia miradi ya maji kwa ajili ya kupunguza shida wanazokumbana nazo wakina mama kutafuta maji. 

"Mh. Raisi , tumejipanga pia kuhakikisha kuwa halmashauri yetu inajiwezesha yenyewe. Zaidi ya Milioni 200 zimepelekwa kuwasaidia wananchi maskini kimikopo na shighuli za maendeleo.  Kushirikiano na wadau wa maendeleo tumefanikiwa katika haya." Mbunge alieleza.

Pia mbunge alimuomba Mh. Raisi kutumia Chalinze kama sehemu ya ushuhuda wa hatua na jitihada anazochukua kukuza uchumi wa watu na maendeleo ya kweli yanayotazama uelekeo wa kiilani na ahadi zake. Mheshimiwa Mbunge alimueleza Mheshimiwa Raisi kuwa ," kama yupo mtu ambaye ana shaka na utayari wako na uchapakazi wako juu ya sera ya viwanda basi Mwambie aje Chalinze aje kuona jinsi mambo yanavyofanyika." Tunajua wewe ni kazi tu na sisi hapa chalinze ni kazi tu. "

Mheshimiwa Raisi alimshukuru Mbunge na kwa hakika alimpongeza kwa kumfananisha na Baba yake Aliyewahi kuwa Raisi Wa Jamhuri ya Tanzania wakati wa awamu ya Nne. Mheshimiwa Raisi alimfananisha na Nyoka mtoto. "Kwa hakika nimemsikia Mbunge wenu na nimeridhika kuwa Nyoka uzaa Nyoka".Nimekuona na nina kuiongoza unavyochapa kazi. Hongera sana ."

Pamoja na kumshukuru mbunge , Mheshimiwa Raisi aliwakabidhi Halmashauri ya Chalinze majengo ambayo yalitumiwa na Mkandarasi pale Msata wakati wa Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Masata.

Baada ya kumaliza mkutano huo na kufungua kiwanda cha kuchakata Matunda cha Sayona, Mheshimiwa Raisi alielekea Bagamoyo ambako alifanya mambo mawili makubwa ikiwemo uzinduZi wa Barabara ya Bagamoyo Msata na Kiwanda cha kukausha Matunda kilichopo Mapinga, Bagamoyo.

*Imeandaliwa na Afisa Habari
  Ofisi ya Mbunge-Chalinze*

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List