DC Hapi atoa vifaa tiba Hospitali ya Mwanayamala
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi leo ametoa vifaa tiba katika Hospitali ya Mwanayamara iliyopo wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli.
Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akitoa vifaa hivyo katika hospitali hiyo, amesema kuwa vifaa hivyo vinagharama ya shilingi milioni 400 ambapo vitasaidia kupunguza changamoto mbalimbali hospitalini hapo.
‘Ndugu zangu vifaa hivi vitasaidia kupunguza changamoto kwa kiasi kikubwa, naomba tu kuwahamasisha wananchi kuungana na Serikali kuweza kusaidia Hospitali zetu sehemu ambapo kila mmoja atafaidika,”amesema Hapi
Hata hivyo, Hapi ameongeza kuwa bado hajaridhishwa na ukusanyaji wa mapato katika huduma ya wagonjwa wa msamaha ambapo Serikali inagharimia fedha nyingi zinakwenda kugharamia wagonjwa wa misamaha kuliko wale wa kawaida.
WAFANYA BIASHARA KARIAKOO WAMLILIA RAIS DKT.SAMIA AWANUSURU KUONDOLEWA
KATIKA ENEO LAO
-
Umoja wa Wafanyabiashara wa Mtaa wa Mahiwa na Zigua Kariakoo Jijini Dar
es Salaam wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati
operesheni ya ...
Saa 6 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni