Ni jambo zuri ukiona mtu wako wa karibu amefanikisha moja ya ndoto zake katika maisha yake. Ni muhimu kumpatia ujumbe ambao utakaomtia moyo katika kufanikisha mambo yake mengine aliyoyapangilia.
Vanessa Mdee ameamua kutumia vizuri fursa hiyo katika kumpongeza mpenzi wake Jux ambaye amehitimu masomo yake huko nchini China. Lakini katika ujumbe huo pia Vee amewapiga dongo watu waliokuwa wakimkejeli mwenza wake huyo kutokana na muimbaji huyo kutoonyesha picha yoyote akiwa na wanafunzi wenzake.
Kupitia mtandao wa Instagram, Vanessa ameandika:
Congratulations @juma_jux U finally done ✅ and you done did it well. Hapo watu walikuwa wakiombaga picha za wewe darasani nadhani hii picha jibu la kutosha. Umeweza kufanya yote, MZIKI, BIASHARA NA SHULE… now that’s exceptional. Muda wa vibunda babaaa. Keep inspiring the YUTEEEEE 🙌🏾👌🏾🎊
WAFANYA BIASHARA KARIAKOO WAMLILIA RAIS DKT.SAMIA AWANUSURU KUONDOLEWA
KATIKA ENEO LAO
-
Umoja wa Wafanyabiashara wa Mtaa wa Mahiwa na Zigua Kariakoo Jijini Dar
es Salaam wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati
operesheni ya ...
Saa 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni