Makonda kumaliza msongamano katika hospitali Dar es salaam
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amekagua wodi ya akina mama katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala Jijini Dar es salaam.
Katika ukaguzi huo Makonda amesema kuwa kukamilika kwa wodi hiyo kutasaidia kuondoa msongamano mkubwa uliokuwepo kipindi cha nyuma hivyo amewaasa wahusika kutunza wodi hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa katika idara ambayo anaamini kuwa itafanya vizuri katika mkoa wa ni sekta ya afya kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakijitolea kusaidia katika sekta hiyo. Pia amewashukuru watu wote waliojitolea kuweza kuchangia hivyo amewaasa wananchi kujitokeza kuungana na Serikali katika kuujenga mkoa wa Dar es salaam.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
Saa 2 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni