KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA IDADI YA WATU DUNIANI MARIE STOPES WAMEENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA NA UTOAJI WA ELIMU KWA WATANZANIA.

Shirika la Marie stopes lenye ofisi zake Mwenge, Dar es salaam linalo shughulika na utoaji wa huduma mbalimbali za afya hususani afya ya uzazi na uzazi wa mpango pamoja na utoaji wa elimu ya afya ya uzazi (sexual and reproductive health education) na haki ya kufanya maamuzi juu uzazi mpango(sexual and reproductive health rights). 

Katika kuzingatia umuhimu wa idadi ya watu wameendesha zoezi la upimaji wa afya bure maeneo ya viwanja vya mwembe yanga, Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani.Lengo ni kutambua hali za afya(Health status) kwa wananchi wa Tanzania ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na maradhi mbalimbali. Hili linaenda sambamba na utoaji elimu juu ya uzazi wa mpango ili kutoa fursa kwa watanzania kupata idadi ya watoto wanaoweza kukidhi mahitaji yao na huduma zote muhimu ikiwemo elimu na afya Marie stopes kupitia kauli mbiu yao(slogan)"watoto kwa utashi si Kwa kubahatisha "Wametawala viwanja vya mwembe yanga huku wakisisitiza Watanzania kujenga mazoea ya Upimaji wa afya na kutumia njia sahihi ya uzazi wa mpango sambamba na kutoa elimu juu ya magonjwa yanayotokana na Ngono isiyo salama na Magonjwa mengine kama saratani ya mlango wa kizazi, magonjwa ya sukari na shinikizo la damu ambapo pia huduma hizo zote hutolewa katika Hospitali ya Marie Stopes Mwenge. 

Mratibu mradi wa kanda ya mashariki na pwani kutoka Marie stopes Alfredy Obeidy Mellah  amesema zoezi la upimaji na zoezi zima kwa ujumla Lina changamoto nyingi ikiwemo watu kutojitokeza kwa wingi ili kuvuka malengo ya watu 2000 kwa siku Tatu, Pia amesema elimu ya uzazi wa mpango bado ni changamoto nchini Tanzania hasa maeneo ya vijijini kutokana na tamaduni na Imani potofu inayohusisha njia ya uzazi wa mpango na uvimbe tumboni pia baadhi ya watu Wana Imani kuzaa watoto wengi ni baraka ndani ya familia. Akimalizia amesema lengo la huduma hii ni kuifikia mikoa yote ya Tanzania na kutoa elimu kwa jamii ili kutambua njia sahihi na utaratibu wa uzazi wa mpango kwa idadi ya watoto wanaoweza kuwahudumia. 

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List