Baraza la kitaifa la michezo nchini Tanzania limevunjwa kufuatia madai ya ufisadi.
Hatua hiyo inajiri wiki mbili tu baada ya maafisa wakuu wa shirikisho la soka nchini humo kushtakiwa na ulanguzi wa fedha.
Kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Awami hatua hiyo ilitarajiwa.
Baraza hilo ambalo linahusika na usimamizi wa michezo nchini humo limetuhumiwa kwa kukosa utendaji.
Akilifutilia mbali baraza hilo, waziri wa michezo Harrison Mwakyembe alisema kuwa kushindwa kwao kuimarisha michezo nchini hakutokani na uhaba wa fedha bali uzembe na kutoijali sekta hiyo.
Pia ameshutumu operesheni za baraza hilo kwa kutawaliwa na ufisadi, madai ambayo aliyekuwa katibu mkuu wa baraza hilo Mohammed Kiganja ameyakana.
"kwanza nataka kusema kwamba hakujakuwa na ufisadi katika baraza hilo.Ufisadi umeshamiri katika michezo kwa jumla. Na ninakubaliana na hilo.Iwapo utaenda katika uchaguzi wa vilabu vya soka kuanzia viwango vya Wilaya hadi kitaifa utaona matatizo haya''.
Kuvunjwa kwa baraza hilo kunajiri wiki mbili tu baada ya rais na maafisa wengine wakuu wa shirikisho la soka kushtakiwa kwa ulanguzi wa fedha.
JAJI MFAWIDHI MAGHIMBI AWAFUNDA WAJUMBE KAMATI ZA MAADILI ZA MAAFISA
MAHAKAMA PWANI
-
Mhe. Jaji Mfawidhi Salma Maghimbi akimshuhudia Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe
Petro Magoti wakati akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili
na...
Dakika 48 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni