Bobi Wine kuapishwa kama mbunge Uganda

Mwanamuziki wa nyimbo za reggae nchini Uganda Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, anaapishwa leo kama mbunge wa eneo la Kyadondo East.
Wine aliwania kiti hicho kama mgombea huru na kuwashinda wagombea wanne ambapo alipata kura 25,659 kati ya kura 33,310 zilizopigwa kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 29 mwezi Juni.

Alisema kuwa anaingia bungeni kama kiongozi na wala si mwanasiasa, kwa mujibu wa gazeti la New Vision.
Chama tawala NRM na upinzani wamekuwa wakimtaka Wine kujiunga nao.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List