Leo kilele cha maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani ambayo yamefunguliwa na Dkt:OTILIA GOWELE ambaye ni Kaimu katibu mkuu wizara ya afya na maendeleo ya Jamii, jinsia, wezee na watoto kwa Niaba ya Naibu Waziri wa afya na ustawi wa jamii, Mashirika Mbalimbali wamejitolea kuendesha huduma za upimaji wa afya na utoaji wa elimu ya namna ya kustawisha idadi ya watu, kupunguza idadi ya vifo vya watoto na watu wazima na uzazi wa mpango kwa Familia bora.
Mgeni rasmi Mheshimiwa Dkt OTILIA GOWELE amesema kauli mbiu ya siku ya idadi ya watu duniani ni "Kutokomeza mimba za utotoni" na kutoa wosia kwa jamii kuwa na utaratibu wa kupanga uzazi(uzazi wa mpango) na kutoa elimu kwa watoto wetu ili kujikinga na mimba za utotoni. Na kuwaomba watanzania wajitokeze kupima afya na kujua maendeleo yao kiafya sababu watu wenye afya ndo chachu ya Ujenzi wa Taifa bora lenye uchumi mzuri na maendeleo ya Jamii.
Siku ya idadi ya watu duniani ilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo ngoma za asili pamoja na washauri ambapo walikuwa wanatoa elimu bure kabisa ya uzazi mpango ili kupunguza kasi ya idadi ya watu na ndoa za umri mdogo (ndoa za utotoni) na masuala yote ya kijamii yenye uhusiano na idadi ya watu. Maadhimisho hayo yatafungwa kesho tarehe 12/07/2017
Mashirika yaliyotoa huduma kikamirifu na kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya afya na ustawi wa jamii kufanikisha maadhimisho hayo ni MARIE STOPES TANZANIA, PSI , Engender Health, USAID, AMREF, PATHFINDER , MDH, PATH , JOHNS HOPKINS, Dkt International, Jhpiego, UMATI, T-MARC TANZANIA, UNFPA na ELIZABETH GLASER PEDIATRIC AIDS FOUNDATION.
0 comments:
Chapisha Maoni