Taarifa ambazo zilizotoka jioni ya July 9, 2017 zilikuwa ni kuhusu kifo cha Seth Katende ambaye alikuwa Mtangazaji wa
EFM akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Leo Seth Katende amezikwa katika Makaburi ya Kinondoni.
Seth Katende alijipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii Tanzania akifahamika kwa jina la ‘Bikira wa Kisukuma’.
Na katika kipindi kilichokuwa kinaruka hewani cha ubaoni wakishirikiana na Mpoki na Emma Kapanga, kutoka redio EFM na kujizoelea umaarufu mkubwa hivyo kupendwa na watu wa rika zote Tanzania.
Tunajua msiba wake ni mkubwa na ameacha majonzi kwa Watanzania wote. Pumzika kwa Amani
0 comments:
Chapisha Maoni