Katika Harakati za kuimarisha chama cha Mapinduzi (CCM) ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ameungana na wanachama wengine katika kikao ambacho kilikuwa na dhamira ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ili kuweka ngome Imara na kusaidia utekelezaji wa Irani ya Chama cha Mapinduzi jimboni Chalinze.
Akiongea na mwandishi wa blog yetu mbunge wa Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amesema "katika Harakati za kuimarisha Chalinze leo nimeshiriki kikao cha Maendeleo cha Chama Cha Mapinduzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Nawashukuru sana Wajumbe na viongozi wenzangu. Ngome Imara ya Maendeleo katika Halmashauri yetu ni CCM. #hapakazitu #magufulinikazitu #chalinzenikazitu
Pia alilisitiza kauli ya hapa kazi tu kama sehemu ya kusaidia kupambana na matatizo mbalimbali ya Chalinze na kusema CCM itaendelea kutawala sababu ni chama chenye dira, uwajibikaji na Irani inayo tekelezeka.
0 comments:
Chapisha Maoni