Rooney awachanganya mashabiki Dar, Mwakyembe atoa neno
Hatimaye mapema leo timu ya Everton imewasili jijini Dar es Salaam kwa lengo la kushiriki mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya.
Wakati timu hiyo ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wachezaji wote walishuka kwenye ndege yao binafsi na kuelekea katika basi lao maalum huku wakipita kila mmoja kumshika mkono mwenyeji wao, Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Dk. Harrison Mwakyembe. Lakini mchezaji mpya wa klabu hiyo, Wayne Rooney alionekana kuwachanganya zaidi mashabiki waliofika uwanjani hapo.
Rooney ambaye alikuwa wa mwisho kushuka kwenye ndege hiyo alionekana kushangiliwa zaidi na mashabiki ambao walisikika wakimpa ujumbe mbalimbali, huku wengi wakimtaka ageuka angalau awapungie mkono.
Hata hivyo, mchezaji huyo alitulia kama anazisikia kelele za mashabiki wake akiwa Goodison Park akiambaa taratibu na mpira. Mchezaji huyo aliyeiahama Manchester Utd hivi karibuni aliendelea kutembea, kumshika mkono Dk. Mwakyembe na kuelekea kwenye gari.
Akizungumza muda mfupi baada ya wachezaji hao kuingia kwenye basi lao, Waziri Mwakyembe aliwataka mashabiki wote walioko uwanjani na majumbani kuendelea kuwa watulivu na kuhudhuria mechi itakayofanyika kesho katika Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
“Hii ni timu kubwa na Tanzania inafarijika sana kwa ujio huu. Niwaambieni tu Watanzania hata ninyi waandishi wa habari, ulinzi umeimarishwa na katika mazoezi yao hataruhusiwa mtu yoyote asiyehusika kwenda,” alisema Dk. Mwakyembe.
Timu ya Everton iliwasili JNIA majira ya saa 2 na dakika 39 na kuelekea hotelini majira ya saa 3 na dakika 10.
KURUI Vs KISARAWE WAKIPIGA MZENGA
-
*Mzenga,Kisarawe*
Timu za soka Kata ya Kisarawe na Kurui jana tarehe 17 Januari 2025
zimetoka sare ya goli moja moja ikiwa ni katika hatua ya kuwania ...
Siku 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni