MHE:RIDHIWANI KIKWETE NDANI YA SPORTSXTRA NDONDO CUP, KAUZU WAAGA MASHINDANO RASMI.

Mheshimiwa Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete Leo ameudhuria Mashindano ya Mpira wa Miguu ya SportsXtra Ndondo Cup yaliyoandaliwa na Cloudsfm na AzamTv.

Picha Toka Juu... Shabiki Mkubwa  wa Timu ya Kauzu Fc Bwana Chief Kauzu akiingia Uwanjani katika Mtazamo wa kipekee

Baada ya kugawa zawadi Mheshimiwa Mbunge Ridhiwani Kikwete alizungumza na Waandishi wa Habari na kuwaasa sana Vijana kutumia fursa ya Mashindano haya kujitangaza na pia kuzishawishi timu kubwa kuja kushiriki kuangalia viwango vinavyoonyeshwa. Pamoja na hayo kuwekeza katika viwanja vya michezo na kudumisha ushabiki wa timu hasa kwa maeneo wanayotoka.

Pia alifanya Mahojiano na Mwandishi wa Azam Tv wakati wa mapumziko. Wakizungumzia mchezo kwa kipindi cha kwanza na kutoa maoni juu ya uelekeo wa mchezo.

Mchezo ulipokwisha Mbunge wa chalinze Ridhiwani Kikwete aligawa Zawadi kwa viongozi wa timu ya StimTosha ya Mabibo ambao ndiyo walioibuka na Ushindi wa Magoli 4-2 kwa njia ya Penalti baada ya kumaliza mchezo kwa sare ya 1-1

nikisaini kitabu cha Wageni

Mchezo huo uliwakutanisha Mheshimiwa Mbunge na aliyekuwa  kapteni  na kocha wa Timu ya mpira ya Simba ambaye yeye mwenyewe hupenda kumuita "kaka yangu Selemani Matola" .

Alipata nafasi ya kuongea na nikifurahi jambo na Chief Kauzu wa Timu ya KauzuFc ya Tandika

Nane ni zawadi kwa timu ya Kauzu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List