Neymar asilimia 90 kuondoka Barcelona
Uwezekano wa mshambuliaji raia wa Brazil Neymar Jr kuondoka katika klabu ya Barcelona ni mkubwa kutokana na mchezaji huyo kutokuwa na furaha ndani ya klabu hiyo.
Kuna taarifa kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anataka kucheza katika klabu nyingine ili aweze kung’ara na kushinda Ballon d’Or kitu ambacho hawezi kufanya Barcelona kutokana na uwepo wa Lionel Messi.
Klabu ya Paris Saint-Germain ndio klabu pekee iliyo tayari kutoa kiasi kikubwa cha pesa ambayo Barcelona wanaitaka ili kumnunua Neymar huku klabu za Chelsea na Manchester United zikiwa haziko tayari kufanya hivyo.
PSG ambao wamekuwa wakimtaka Neymar kwa kipindi kirefu sasa wako tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 196 ili kumsajili mshambuliaji huyo.
Taarifa zinasema Barcelona wamekuwa wakimtaka Neymar kukana kwa Uma taarifa za kuwa hana furaha katika klabu hiyo lakini mchezaji huyo hajafanya hivyo.
Upo uwezekano wa Neymar kuondoka Barcelona na kuna taarifa kuwa amewaambia rafiki zake wa karibu jambo hilo.
Wakati huohuo raisi wa klabu ya Barcelona Josep Bartomeu amesema Neymar hauzwi.
ASHA BARAKA ATOA NENO LA SHUKRANI KWA H/KUU CCM
-
Asha Baraka ametoa shukrani zake za dhati kwa Kamati ya Halmashauri Kuu
Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumteua kuwa mmoja wa wagombea
Ubung...
Saa 11 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni