Mbunge wa Chalinze leo amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo la chalinze zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya bagamoyo.
Pamoja na kugawa jezi , mbunge wa chalinze aliwaahidi kuwapatia mshindi wa pili wa mashindano Pilkipiki ya Miguu miwili, na jezi kwa timu zote Tatu za juu kufuatia mkuu wa wilaya kuwachangia mshindi wa kwanza pikipiki ya Toyo ya miguu mitatu ili itumike kwa shughuli za kipato kwa vijana.
Sherehe hizo zilizofanyika kimange zilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Madiwani wote wa Jimbo la Chalinze na watendaji wao wa kata ambao walipokea jezi kwa niaba ya timu zao. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye muandaaji mkuu wa mashindano hayo akishirikiana na wabunge wa majimbo yote
KISARAWE KURINDIMA NUSU FAINALI JAFO CUP
-
Timu nne zinatarajiwa kushuka dimbani mwishoni mwa wiki ikiwa ni katika
mchezo wa nusu fainali ya michuano inayoendelea ya 'Jafo Cup' Wilayani
Kisarawe ...
Saa 14 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni